WAMENASWA! Jeshi la Polisi Kituo cha Buguruni kwa kushirikiana
na Serikali ya Mtaa wa Machimbo, Kata ya Segerea, Ilala jijini Dar es
Salaam wamewanasa watu 105 raia wa Somalia wakidaiwa kuwa safarini
kwenda nchini Afrika Kusini, Uwazi linakupa kwa undani.
Tukio hilo la kushangaza lilitokea saa 11 alfajiri ya Alhamisi
iliyopita kwenye nyumba ya kigogo mmoja aliyekuwa mfanyabiashara mkubwa
Dar (jina lipo) ambaye ni marehemu. Nyumba hiyo iliyopo Tabata Segerea
kwa sasa inasimamiwa na mtoto wa marehemu aitwaye Mariam.
Polisi wakiwa katika eneo la tukio.
Waadishi wa habari hii walifika eneo la tukio muda mfupi baada ya
kukamatwa kwa watu hao ambapo zoezi hilo lilikuwa likiongozwa na Mkuu wa
Upelelezi Wilaya ya Kipolisi Buguruni, Ibrahim Nkindwa na Mkuu wa Kituo
cha Polisi Tabata Shule, Bakar Goti baada ya kutonywa kuwepo kwa watu
hao katika nyumba hiyo iliyopangishwa kwa Zabibu Umwiza raia wa Burundi
ambaye ndiye anadaiwa kuwahifadhi watu hao.
ainabu alikimbia baada ya polisi kufika na silaha za moto.
Kwa mujibu wa shuhuda mmoja, kugundulika kwa Wasomali hao kulifuatia
kuwasili kwa lori moja kwenye nyumba hiyo usiku wa saa tisa.
….Wakiwa kwenye basi la polisi.
“Baada ya lori kufika usiku huo, geti likafunguliwa. Halafu kukaanza
kusikika vishindo vya tii…tii…tii! Kumbe jamaa (Wasomali) walikuwa
wakiruka chini mmojammoja kutoka kwenye lile lori na kuingia ndani.
“Ndipo jirani mmoja aliamua kutoa taarifa polisi ambao walifika na
kuwakuta jamaa wamerundikana ndani kwenye vyumba tofauti. Mia moja na
tano ni wengi sana,” alisema shuhuda huyo.
0 comments:
Post a Comment