
TAASISI
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilayani Igunga mkoani Tabora, imemfikisha mahakamani daktari Salumu Rashidi
(58) aliyegoma kumtibu mtoto wa miaka miaka miwili.
Mwendesha
mashitaka wa taasisi hiyo, Aidan Samali alimsomea Rashidi shitaka lake mbele ya
Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Igunga, Ajali Milanzi.
Samali
alidai mahakamani hapo kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Desemba 21, mwaka
huu, katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora.
Alidai
kuwa Rashidi ni mtumishi wa hospitali
hiyo anadaiwa kuomba rushwa ya sh. 40,000 kutoka kwa Gigwa Malale mkazi
wa Kijiji cha Mgongoro ili aweze kumpatia matibabu mwanawe Nkamba Mbusule
aliyekuwa ameingiwa na punje ya mahindi puani.
Ilidaiwa
mahakamani hapo kuwa mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha
15 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa ya mwaka 2007, kinachozuia
kutenda makosa kama hayo.
Hata
hivyo, Rashidi alikana shitaka lake na kurudishwa mahabusu baada ya kukosa
mdhamini. Kesi hiyo itatajwa tena Januaria 11, mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment