Ikiwa imepita miezi kadhaa tangu staa wa Muziki wa Bongo Fleva,
Estalina Sanga ‘Linah’ aachane na mchumba wake, amekiri kutakwa
kimapenzi na mastaa wa muziki nje ya nchi (Afrika).
Akichonga na Amani Linah amesema, mara nyingi amekuwa akisumbuliwa
kimapenzi na mastaa wengi wa muziki Afrika lakini hakuwa tayari kuwaweka
wazi na wala kutaja kama alishawahi kubanjuka na mmoja wapo kati ya
hao.
“Ni kweli wapo wengi walionitaka kimapenzi, lakini itabaki kuwa siri
yangu kujua ni wangapi na nilimkubalia nani kati ya hao,” alisema Linah.
0 comments:
Post a Comment