WAZIRI
Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye, ameiangukia serikali na kuomba msaada
baada ya wananchi kuchukua sheria mkononi na kuvamia eneo lake la ekari
33 lililopo Mabwepande katika Manispaa ya Kinondoni nje kidogo ya jiji
la Dar es Salaam.
Serikali
imemuahikikishia Sumaye kuwa haina mpango wa kumkandamiza mtu mnyonge
wala tajiri hivyo itahakikiha inatoa haki kwa kila mmoja baada ya wiki
mbili kwa kua imesikiliza pande zote mbili katika mgogoro huo.
Akizungumza
katika kikao cha pamoja kati ya wananchi wa kitongoji cha Kimondo mtaa
wa mji mpya Kata ya Mabwepande na Sumaye Dar es Salaam leo asubuhi,
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda alisema ili kumaliza mgogoro
huo ambao Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye ameiomba serikali
kuingilia kati ni lazima busara kutumika.
Alizitaka
pande hizo mbili kuiachia serikali kwa wiki mbili ili kutafuta njia
bora ya kumaliza tatizo hilo huku wananchi wakitakiwa kuache kuendelea
na ujenzi na kugawiana maeneo katika shamba hilo.
“Serikali
ya Rais Magufuli ni sikivu na ndio maana ilikuwa tayari kumsikiliza
Waziri Mkuu wetu Mstaafu Sumaye na kusikiliza wananchi ili kutenda haki
tunatambua migogoro ya ardhi ilivyokuwa na athari kwa jamii hatuna
mpango wa kumkandamiza tajiri wala mnyonge,”alisema.
Alisema
katika eneo hilo anajua jinsi wananchi walivyotumia nguvu katika
kuwekeza ujenzi na rasilimali zao lakini kwa sasa wasitishe shughuli
hizo na kuendelea kugawana maeneo na Sumaye pia kuacha uwekezaji ili
kutafuta suluhu.
Zipo
njia nyingi tutazitumia kumaliza mgogoro huu ikiwemo kufuata sheria kwa
kuangalia iwapo mzee wetu alikiuka taratibu kweli za kumiliki ardhi
kama ilivyodaiwa na wananchi hatua gani serikali tuchukue,”alisema.
Alisema
pia wanaweza kukaa na Sumaye na kuzungumza naye ili kukubali hasara kwa
kutoa eneo kidogo na kuwapatia wananchi hao ambao hawana makazi au
Manispaa kutafuta eneo mbadala na kuwauzia kwa bei nafuu.
Alizitaka
pande hizo mbili kutambua umuhimu wa kulinda amani katika mgogoro huo
kwa changamoto zilizopo kutatuliwa bila kutumia nguvu.
Makonda pia aliagiza serikali ya kijiji kufanya utambuzi wa wananchi hao wenye makazi katika shamba la Sumaye.
Awali
katika mkutano huo Sumaye alimueleza Makonda jinsi serikali ilivyo na
kazi ngumu ya kushughulikia migogoro ya ardhi na kuomba kutumia busara
zake kumpatia eneo hilo analomiliki kihalali.
“Mheshimiwa
Mkuu wa Wilaya kama nilivyokueleza awali serikali yetu inakazi ngumu
sana hasa kutokana na viongozi wa chini kutokuwa wasikivu na wakweli
eneo hili namiliki kihalali nina nyaraka zote na ninalipia kila mwaka na
nilikuwa katika mpango wa kutafuta wafadhili ili kuliendeleza kwa
kujenga Chuo Kikuu,”alisema.
Alisema yeye na familia yake waliuziwa eneo hilo toka mwaka 1997 na anaamini serikali itatenda haki.
Diwani
wa kata hiyo Suzan Masawe alisema anauthibitisho kuwa eneo hilo
lilikuwa pori na Sumaye alilitelekeza kwa muda mrefu na kusababisha
uhalifu ikiwemo wanawake kubakwa,mali za wizi kufichwa na uhalifu
mbalimbali.
Alisema
kutokana na hatua hiyo walimtafuta Sumaye lakini hakuwa na
ushirikiano kwakuwa hata alipofanya uwekezaji kwa kuchimba kisima cha
maji alikataa kuwapa wananchi .
Suzan
alisema kutokana na hasira za wananchi hao kwa kukosa huduma za kijamii
kwa muda mrefu ikiwemo eneo hilo kutokuwa na shule,Zahanati wala kituo
cha polisi waliamua kuvamia na kujigaia maeneo.
Mmoja
wa wananchi hao Athuman Mnubi alikiri kweli hawana umiliki halali wa
eneo hilo na katika hatua ya kutafuta makazi walivamia msitu huo
uliotelekezwa na Sumaye.
Alisema
wanaamini kutokana na ahadi ya serikali ya Rais Magufuli katika kupora
maeneo yaliyotelekezwa na wawekezaji watasaidiwa.
0 comments:
Post a Comment