Sunday, January 10, 2016

Mwimbaji wa Bandi ya Skylight, Suzy wakiwapa raha mashabiki wa Skylight Band (hawapo pichani) uku akisindikizwa na Natasha(kulia) pamoja na Leah ndani ya kiota cha Escape One jumapili iliyopita sasa leo sio siku ya kukosa njoo ujionee mambo mapya kutoka kwenye bandi ya Skylight.
Sam Mapenzi akiongoza marapa wenzake wa Skylight Band, Suzy na Sony Masamba kutoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band Jumapili iliyopita ndani ya kioa cha Escape One Mikocheni ambapo leo pia burudani iko pale pale na ndio kwanza week end imeanza kwa fans wa Skylight Band.
Waimbaji wa bendi ya Skylight, Joniko Flower na Sony Masamba wakiendelea kutoa burudani mbele ya mashabiki wao ndani ya kiota cha Escape One Mikocheni jijini Dar.
Mashabiki wakiendelea kusebeneka na burudani ya Skylight Band.
 Rapa Mkongwe wa muziki wa dansi wa Skylight Band, Joniko Flower akiwasebenesha sehemu ya mashabiki pamoja na waimbaji wa bendi hiyo ndani ya Jumapili iliyopita kwenye Skylight Sunday Bonanza‬ kiota cha Escape One Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Mwananziki wa bendi ya Skylight Sony Samba akiimba moja ya sebene la bendi hiyo uku waimbaji wa Skylight wakendelea kuserebuka ndani ya Kiota cha Escape One Mikocheni
Tofe aka 2be ambaye ni Mpiga Bass akiendelea kuwakonga nyoyo mashabiki wao katika kiota cha Escape One Mikocheni Jumapili iliyopita.

0 comments:

Post a Comment