| Dr. Kiiza Besigye. |
MGOMBEA urais nchini Uganda kwa tiketi ya chama cha
Forum for democratic change-FDC Dr. Kiiza Besigye, ametoa changamoto
kwa mwenzake wa chama tawala cha National resistance movement-NRM rais
Yoweri Museveni, kutokwepa mdahalo wa pamoja wa wagombea wote wa urais
unaotarajiwa kufanyika siku ya Ijumaa wiki ijayo...,
Besigye alikuwa akihutubia umati mkubwa wa watu
mashariki mwa Uganda katika mji wa Mbale akiwa kwenye uwanja mmoja mjini
humo uliojaa watu kupita kiasi.
Mdahalo huo umeandaliwa na taasisi za kidini na Besigye anasema itawapa wananchi wa Uganda kuchambua mbivu na mbichi kisiasa.
0 comments:
Post a Comment