Monday, January 18, 2016

Blogu ya Wananchi imejulishwa muda mchache uliopita kwamba kuna habari za kusikitisha asubuhi hii za kifo cha ghafla cha Mkurugenzi wa Viwanja vya ndege Tanzania Bw. Selemani ambaye anasemekana kuwa na tabia ya kuogelea kwenye Club yake ya kuogelea iliyopo Ferry kabla ya kufikia kivuko cha kuelekea Kigamboni karibu na mwisho wa kona ya Ikulu hapa mjini Dar. Blogu hii ya Wananchi imefahamishwa kwamba Marehemu alikuwa na tabia ya kushirikiana na wanachama wenzake wa Club hiyo kuvuka pande mbili kwa kwenda Kigamboni na kurudi Posta mara tatu kila siku Asubuhi kwa kuogelea. Leo pia akiwa katika mpito huo wa kawaida alipatwa na Heart Attack akiwa kati kati ya Bahari akiwa njiani kuelekea Kigamboni na kufariki Dunia hapo hapo......... Habari zaidi zinakuja soon

0 comments:

Post a Comment