KUTOKA TAKUKURU
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Kamishna wa Polisi Valentino Mlowola amefanya mkutano na Waandishi wa Habari leo na kueleza dhamira ya TAKUKURU ya kupeleka mahakamani kesi 36 zinazohusisha ukwepaji kodi na rushwa.
Katika kesi hizo moja inaihusisha Kampuni ya Mafuta ya Lake Oil. Katika shauri hili kampuni hii ilifanya udanganyifu kuwa ilisafirisha mafuta aina ya Petrol lita 17,461,111 kwenda nchini Congo (DRC) kupitia Zambia.
Kamishna Mlowola amesema TAKUKURU imekamilisha uchunguzi wake juu ya suala hili na kubaini kwamba mtuhumiwa (Lake Oil) hakusafirisha mafuta hayo nje ya nchi bali aliyauza nchini na kufanikiwa kukwepa kodi kiasi cha Shilingi Bilioni 8.5
TAKUKURU imemuagiza mtuhumiwa (Lake Oil) kulipa fedha hizo ndani ya siku sitini (miezi miwili) kuanzia leo, na kumpa onyo kwa kufanya udanyanyifu ulioikosesha serikali mapato.
Aidha Mlowola ameongeza kuwa tayari Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imejulishwa na TAKUKURU kukusanya fedha hizo ndani ya miezi miwili na ikiwa Mtuhumiwa (Lake Oil) atashindwa kufanya hivyo atapandishwa Mahakamani kujibu mashtaka ya UHUJUMU UCHUMI, kosa ambalo adhabu yake ni kufilisiwa ikiwa atapatikana na hatia.
#MyTAKE.!
JPM utamuua Mkwere kwa pressure. Unagusaje Lake Oil kibabe hivi? Kwani alipokukabidhi ofisi hakukuambia ni kampuni ya "Festi boni" wake?? 😆😆

0 comments:
Post a Comment