Waziri
Mkuu alitoa onyo hilo jana wakati alipotembelea Hospitali hiyo na
kuzungumza na watumishi kwa lengo la kuwasisitiza kutoa huduma bora kwa
wagonjwa,ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku 3 mkoani Ruvuma.
Alisema Hospitali ya mkoa huo inasifika kwa kutoa mimba wanawake na kuwalaza wagonjwa wao wodi namba 5, kitendo ambacho serikali haikuruhusu wala haikubaliani nacho.
"Naomba
mkuu wa mkoa fanya ziara ya kushtukiza katika wodi namba 5 utakuta
wanawake wametolewa mimba, wakiwemo wanafunzi na kisha madaktati hao
wanatumia wodi zetu kuwalaza wagonjwa wao waliowatoa mimba.Ni marufuku
na nitawachukulia hatua kwani majina ya madaktari hao ninayo," alisisitiza majaliwa.
Waziri
Mkuu Majaliwa alimuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa huo,Dr. Daniel Malekela na
Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Dr. Phils Nyimbi kuwafuatilia
madaktari wanaojihusisha na vitendo hivyo na kutoa taarifa ili
wachukuliwe hatua kali.
Pia, alimuagiza
mganga mkuu Dkt Daniel Malekela kuondoa duka lake lililo jirani na
hospitali hiyo ili kuondo hisia kwamba dawa zinaibiwa na kupelekwa
kwenye maduka ya watumishi.
0 comments:
Post a Comment