Mamlaka
ya mapato nchini TRA mkoani Morogoro imekamata madumu 1,599 ya mafuta
ya kula aina ya OKI yaliyokua yakisafirishwa kwenda nje ya nchi bila
kulipiwa ushuru.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake meneja wa TRA mkoa
wa Morogoro Philip Kimune amesema wamekamata shehena hiyo ya mafuta
baada ya kupitishwa nchini kwa njia za magendo na hayakuwa yamelipiwa
kodi halali ya TRA ambayo ni shilingi milion 64.7 hivyo kuamua
kuutaifisha mzigo huo.
Baada ya kukamatwa kwa mafuta hayo, TRA mkoa wa Morogoro
wamewasiliana na ofisi ya kamishna wa forodha na kupewa jukumu la
kuyagawa mafuta hayo kwa taasisi za serikali sambamba na vituo vya
watoto yatima ambapo kwa upande wa magereza mkoa wa Morogoro wamepata
madumu 804, hospitali ya mkoa wa Morogoro madumu 480 sambamba na vituo
vingine vya watoto yatima ambavyo vitagawana madumu 105 kwa kila mmoja.
Wanufaika wa mgao huo waliofika mapema kuchukua mafuta hayo wametoa
shukrani zao kwa mamlaka ya mapato Tanzania TRA kwa kuwakumbuka ambapo
ASP Zephania Neligwa akizungumza kwa niaba ya gereza la mahabusu la
mjini Morogoro amesema badokuna uhitaji mkubwa wa msaada kwa maeneo kama
hayo.
0 comments:
Post a Comment