WAZIRI Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba, amesema mgogoro wa kisiasa unaoendelea sasa visiwani Zanzibar ni tatizo la kitaifa.
Kauli hiyo aliitoa jana wakati wa kongamano la saba la Jumuiya ya
Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), lililofanyika katika
Ukumbi wa Nkrumah chuoni hapo.
Jaji Warioba ambaye pia ni rais wa jumuiya hiyo, alisema yapo masuala
ya msingi yanayotakiwa kubebwa kitaifa badala ya kuyafanya ya kisiasa
na mojawapo ni mgogoro wa kisiasa wa Zanzibar.
“Zanzibar ni tatizo la kitaifa sio la kisiasa, tulifanye kitaifa ili liweze kutatuliwa,” alisisitiza Jaji Warioba.
Alisema kuna jazba katika masuala ya uchaguzi na pia ziliibuka wakati
wa kukusanya maoni ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo alikuwa
Mwenyekiti wake.
“Hili wananchi walilizungumza sana na tulilifanyia tathmini,
tuliamini hata iundwe tume gani bado hupati matokeo sahihi, kama huondoi
rushwa, udini, ukanda huwezi kuwa na uchaguzi huru na wa haki,” alisema
Jaji Warioba.
Alisema suala la rushwa nalo linapaswa kuangaliwa kitaifa na
kushughulikiwa tangu wakati wa uteuzi wa wagombea ndani ya chama ili
kuweza kupata uchaguzi huru.
“Rushwa ni tatizo la kitaifa, hivi sasa Chadema kinaangalia CCM na
CCM kinaangalia Chadema hilo ni tatizo,” alisema Jaji Warioba.
Naye mwanazuoni nguli, Profesa Issa Shivji, alizungumzia suala la kupinga urais mahakamani linapaswa kuruhusiwa kisheria.

0 comments:
Post a Comment