Dully Sykes amesema licha ya kutembea na wanawake wengi, mpaka sasa bado hajapata mke mwema wa kumuoa.
Muimbaji huyo mwenye watoto wanne, amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio kuwa akipata mke mwema ataoa.
“Sijapata mke, unajua mke si girlfriend material na kuna wife material,” alisema. “Sijali Mungu hajaniletea mke na ukifa bila mke si dhambi kwa sababu hakukuletea alitaka ufe bila kuoa. Wife material akiona watu hawezi kushangaa shangaa. Mke anajua kesho unaingia kazini saa ngapi na utakwenda kumpokea saa ngapi. Hawa wanawake wa kwenye show wengine hata sio ma-girlfriend material.”


0 comments:
Post a Comment