Sunday, January 17, 2016

BAADA ya kulisakama kwa muda mrefu hatimaye Serikali kupitia Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nauye, imelifungia kwa muda wote gazeti la kila wiki la MAWIO
linalochapishwa na kampuni ya Victoria Media Services Ltd. 
Katika tangazo lake lililotolewa kupitia gazeti la Serikali notisi namba 55 ya Januari 15, 2016 Serikali imebainisha kuwa imechukua uamuzi huo wa kulifungia gazeti la Mawio kwa muda wote kwa mujibu wa mamlaka iliyonayo kupitia sheria ya magazeti ya mwaka 1976 sura ya 229 kifungu cha 25(1).
“Mawio linatakiwa kusimamisha uchapishaji wake kwa kipindi chote ikiwemo pia katika vyombo vya mawasiliano vya kielektroniki kuanzia Januari 15, 2016”, ilisema sehemu ya tangazo hilo ambalo limetolewa katika gazeti la serikali, likisainiwa na waziri Nape Nauye.

0 comments:

Post a Comment