| Mkuu wa Idara ya Usafi na Mazingira jiji la Arusha ,James Lobikoki |
Wananchi
wa Mtaa wa Matejo uliopo jijini Arusha wameiomba serikali iwapatie
mikopo ili waweze kufanya shughuli mbadala za kujiingizia kipato badala
kujishughulisha na uuzaji wa pombe haramu ambazo zinadaiwa kuwa sababu
ya kuenea kwa kipindupindu.
Wananchi hao wakizungumza katika operesheni ya tokomeza kipindupindu iliyoendeshwa na Ofisi ya Mkuu wa wilaya kwa kushirikiana na Halmashauri na kamati ya Ulinzi na usalama wameteketeza mitambo ya kupikia pombe hizo aina ya piwa, dadi na chang`aa ambazo pia
huathiri afya za watu.
Ester Stephano Shaka ambaye ni Muuzaji wa pombe hizo na Wilfred
Lyakimu na wamesema kuwa maisha yao yanategemea biashara ya pombe za
kienyeji ambazo huwasaidia kusomesha watoto na kupata mahitaji ya
nyumbani hivyo ameiomba serikali iwapatie mikopo ili waweze kufanya
biashara mbadala badala ya kutumia nguvu kutokomeza biashara hiyo.
Mkazi wa Matejo Jovan George amesema kuwa kutokana na tatizo la ajira
limewapelekea watu wengi kujiingiza katika biashara hiyo na matumizi ya
pombe hivyo ameitaka serikali kutafuta njia mbadala.
Mkuu wa Idara ya Usafi na Mazingira jiji la Arusha ,James Lobikoki
amesema kuwa uteketezaji wa pombe haramu ni moja kati ya jitihada
wanazozifanya katika utekelezaji wa operesheni tokomeza kwani kutokana
na mazingira machafu ya uandaaji wa pombe hizo kwani zoezi hilo ni
endelevu.
Ugonjwa wa kipindupindu umeenea katika maeneo mengi nchini tayari
wananchi wameanza kuchukua tahadhari ya kuweka mazingira safi licha ya
baadhi ya maeneo kukithiri kwa uchafu hivyo kukwamisha jitihada za
kutokomeza ugonjwa huo.
0 comments:
Post a Comment