SIKU tatu baada ya Nabii T.B. Joshua wa Nigeria kuonya kuongezeka kwa
nguvu za kijeshi za Korea Kaskazini, nchi hiyo iliyo chini ya utawala
wa Kikomunist, imejaribia kwa mafanikio bomu la haidrojeni.
Joshua alikuwa ametoa wito wa kumwombea
kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-Un, katika ujumbe wake wa Mwaka
Mpya ambapo alifichua utabiri wake Jumapili iliyofuata, Januari 3 mwaka
huu.

Rais wa Korea Kaskazini, Kim Jong – Un.
“Ninaona mshale kutoka huko na utaiathiri dunia,” alisema Joshua na
kuongeza, “inatubidi tuishi kwa amani kwani vita tunavyopigana nchini
Syria bado vinaendelea. Tusitake kuongeza vita vingine tena.”
Kiongozi huyo wa kidini alielezea zaidi silaha zinazoshikiliwa na
taifa hilo akisema “kuna silaha huko ambazo dunia haizifahamu. Nchi
hiyo ikirusha mshale huo, dunia itakanganyikiwa.”
Siku kadhaa baadaye, siku ya Januari 6, nchi hiyo ilitangaza kufanya
jaribio “lililofanikiwa” la bomu la haidrojeni, jambo linaloongeza
wasiwasi dhidi ya nchi hiyo iliyopigwa marufuku kulimbikiza silaha za
nyuklia
0 comments:
Post a Comment