Maafisa wa afya nchini Uingereza
wanatarajiwa kutoa mwongozo mpya kuhusu unywaji pombe, ambapo
watapendekeza watu kutokunywa pombe angalau siku mbili kwa wiki.
Mwongozo huo utatolewa baada ya kutathminiwa upya kwa mwongozo wa awali uliotolewa miaka 20 iliyopita.
Ripoti
zinasema afisa mkuu wa matibabu Uingereza Sally Davies atapendekeza
watu wawe wakijizuia kunywa pombe angalau siku mbili kwa wiki.
Kiwango salama cha wanaume kunywa kwa siku pia kitapunguzwa na kufikia kilichopendekezewa wanawake.
Kwa
sasa, wanawake hushauriwa kutokunywa zaidi ya vipimo 2-3 (sawa na
gilasi ya mililita 175 ya mvinyo) kwa siku na wanaume vipimo 3-4.
Kipimo kimoja cha kileo ni sawa na nusu painti ya pombe isiyo kali sana au lager ya 4.5%, au mililita 25 za pombe kali.
Gilasi moja ya mililita 175 ya divai ya ukali wa 12% ina vipimo 2.1 na painti ya bia kali (ABV 5.2%) ina vipimo vitatu.
Kwa mujibu wa ripoti katika vyombo vya habari Uingereza, mwongozo huo
mpya utasisitiza kwamba hakuna unywaji pombe “salama” na kwamba hata
kunywa viwango vidogo vya pombe kunaweza kusababisha saratani.
Mwongozo nchini Scotland tayari hushauri watu kujizuia kunywa pombe angalau siku mbili kwa wiki.
Mwongozo
huo wa unywaji pombe ulianzishwa 2013 baada ya Idara ya Afya Uingereza
kusema ilikuwa imepokea “malalamiko” kutoka kwa wataalamu wakipendekeza
uchunguzi wa kina kuhusu pombe na afya.

0 comments:
Post a Comment