WAZIRI wa kilimo mifugo na Chakula,Mhe
Mwigulu Nchemba usiku wa kuamkia leo amefanya ziara ya ghafla na ya
kushtukiza katika machinjio ya nyama Vingunguti jijini Dar es Salaam.
Katika ukurasa wake rasmi wa
twitter,Mwigulu amesema kuwa lengo la ziara yake hiyo lilikuwa ni kwenda
kujionea mwenyewe jinsi Serikali inavyopoteza mapato katika sekta hiyo
ambapo amebaini kuwa zaidi ya mapato ya ng’ombe 1107 huishia mifukoni
mwa wajanja.





0 comments:
Post a Comment