Makamu
wa Rais wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan jana jioni aliwasili
mkoani Geita na akakutana na uongozi wa mkoa huo ambapo alisisitiza
suala la wananchi kunufaika na mgodi wao wa dhahabu wa Geita Gold
Mine.…
"Wakati
nilipopita kwenye kampeni nilipita kwenye mgodi wa Geita Gold Mine
nikaangalia hali ya watu wa Geita nikawa na majonzi makubwa…sikuridhika
kuwa na mgodi mkubwa kama ule na hali ya watu wa Geita iko ilivyo hivi
nikawa sikuridhika nilikuwa mkali kidogo." Alisema Mama Samia na kuongeza;
"Wakati
naangalia presentation nimeona amount nzuri kidogo inatolewa kwenda kwa
watu ingawa bado ninamaswali yangu ambayo nitayafanyia kazi ili tuone
ni kiasi gani sahihi kinatakiwa kutolewa na mgodi kwenda kwa wananchi,
dhahabu iliyopo niyawana Geita Mungu amewaumbia katika ardhi yao
"Hatukatai
kuwa na wawekezaji wachimbe lakini uchimbaji uwe na faida kote wao
wapate na wananchi wapate kwa hiyo hatunabudi kusimamia vizuri na
kuhakika kwamba wananchi wa Geita wanafaidika na rasilamali ambayo
Mwenyezi Mungu amewapangia."

0 comments:
Post a Comment