POLISI wilayani hapa, jana walilazimika kumtoa kwa nguvu nje ya
ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero, mbunge wa jimbo hilo,
Peter Lijualikali (Chadema) baada ya kukaidi agizo la mwenyekiti wa
kikao.
Mwenyekiti wa kikao hicho cha uchaguzi wa mwenyekiti wa baraza la
halmashauri ya wilaya na kuapishwa madiwani, Yahya Nania, aliamuru
mbunge huyo atoke kutokana na kutokuwa mjumbe halali wa kikao hicho.
Hatua ya kumtoa nje ya ukumbi ulichukuliwa baada ya kuwepo kwa barua
ya maelekezo ya kisheria kutoka Wizara ya nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI)
kupitia Katibu Mkuu wake yenye kumbukumbu namba CB: 126/443/01/37 ya
Januari mwaka huu ilitoa ufafanuzi wa kisheria kuhusu suala hilo.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyopo katika barua hiyo ilitoa ufafanuzi wa
waziri mwenye dhamana, mbunge huyo amekuwa na nafasi mbili ya Diwani wa
Kata ya Ifakara na pia Mbunge wa Kilombero na hivyo anapaswa kupiga kura
katika baraza la mji mdogo ambako ni mwakilishi na si katika baraza la
halmashauri ya wilaya hiyo.
Kufuatia maelekezo ya kisheria ya Tamisemi, Mwenyekiti wa kikao hicho
alimtaka mbunge huyo asishiriki kupiga kura na kama alihitaji kuwepo,
ajihesabu ni mmoja wa washiriki ama watazamaji katika kikao hicho, jambo
ambalo mbunge huyo alilipinga na kuanzisha vurugu huku akisema kamwe
hawezi kutoka nje.
Mwanasheria wa halmashauri hiyo, Faraja Nakua alisema sheria ziko
wazi na kuwaambia kuwa mbunge wa viti maalumu anapangiwa na chama chake
eneo la kuhudumu.

0 comments:
Post a Comment