Posted by Williammalecela.com on Thursday, January 28, 2016
Couple ya mwanadada mahiri kwenye Tasnia ya Filamu Wema Sepetu na aliyekuwa mshindi wa Big Brother Afrika Idris Sultan, imekuwa Couple inayoongelewa sana barani Afrika, mpaka kufikia hatua ya kuripotiwa na vyombo vya habari vya kimataifa.
Hivi karibu mshindi huyo wa BBA aliandika ujumbe mzito wa kimapenzi unaoonesha hisia zake kwa mwanadada Wema Sepetu kama Mama Kijacho mtarajiwa, ujumbe ambao ulizua gumzo sana kwenye mitandao ya kijamii.
Wema Sepetu nae ameamua kutokaa kimya baada ya kuamua kuandika kwenye ukurasa wake wa Instagram maneno matamu ya kimapenzi yanaashiria kiasi gani anampenda na kufikia hatua ya kumuomba Mwenyezi Mungu awajalie wadumu katika mahusiano yao,
Wema Sepetu ameandika maneno yote hayo, ikiwa ni kuonesha furaha na ushirikiano kwa mpenzi wake kwenye siku yake ya kuzaliwa, ambapo ni jukumu lake kufanya hivyo ili kumfurahisha mpenzi wake Idris Sultan
0 comments:
Post a Comment