Maafisa wa polisi katika mji wa
Cleveland, Ohio, wamewafuta kazi maafisa sita waliowafyatulia risasi
zaidi ya watu 100 katika gari na kuwauwa wachumba wawili weusi mwaka
2012.
Maafisa waliofutwa kazi ni Michael Brelo, aliyeondolewa mashtaka ya kuuwa bila kukusudia mwaka uliopita.
Maafisa wengine sita watasimamishwa kazi kwa siku 21 hadi 30.
Ufyatuaji huo unafuatia msako uliohusisha magari ya polisi 62 na Zaidi ya polisi 100.
Steve Loomis, rais wa chama kikubwa cha polisi mjini humo amesema atapinga kufutwa kazi kwa maafisa hao.
Kisa
hicho kilianza wakati gari bovu lilianza kutoa mlio kama wa risasi.
Ilisababisha kifo cha Timothy Russell, aliyepigwa risasi 24 na Malissa
Williams,aliyepigwa 23.
Maafisa kadhaa walifyatua lakini ni Brelo ndiye aliyeshtakiwa.

0 comments:
Post a Comment