Wakati
watanzania wanasheherekea kuingia kwa mwaka mpya kamanda wa polisi
mstaafu kanda maalum ya Dar es Salaam kamishina mstaafu Suleimani Kova
amekabidhi rasmi wadhifa huo kwa naibu kamishina Simon Sirro katika
hafla fupi iliyo fanyika katika viwanja vya chuo cha maafisa wa jeshi
hilo Kilwa road jijini Dar es Salaam baada ya yeye kustaafu kwa mujibu
wa sheria.
Katika hafla hiyo ambayo imeambatana na maonyesho ya vitu
mbalimbali ambavyo vimekamatwa katika uongozi wake zikiwemo nyara za
serikali, silaa nzito, magari, pikipiki mabomu, nyavu na kuwatunukia
zawadi askari na raia ambao wamefanya kazi nzuri za kufichua uhalifu,
ambapo ameishukuru jamii, familia yake pamoja na vyombo vya habari kwa
ushirikiano mzuri walio mpatia katika utekelezaji wa majukumu yake
ambayo ameyataja kuwa hayakuwa rahisi.
Kwa upande wake kamanda mpya wa jeshi la polisi kanda maalum ya Dar
es Salaam naibu kamishina Simon Sirro amewataka askari polisi wa kanda
hiyo kuachana na vitendo vya rushwa na kusisitiza yeyote atakaye kiuka
taratibu za jeshi hilo hatua kali za kisheria ikiwemo kufukuzwa kazi
zitachukuliwa juu yake.
Katika hatua nyingine kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Ilala ambaye
amehudhuria hafla hiyo amesema jeshi hilo kwa ujumla limejipanga katika
kuhakikisha sherehe za mwaka mpya zinapita kwa amani na utulivu huku
wafanya biashara wa china wakikabidhi pikipiki 3 kwa jeshi hilo kituo
cha Msimbazi ambacho kipo chini ya kamanda huyo.
0 comments:
Post a Comment