JUMUIYA ya mabaharia hapa nchini, jana wamekusanyika Makao Makuu ya Wizara ya Uchukuzi wakidai kupewa
mikataba ya ajira pamoja na kuboreshewa maslahi yao.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es
Salaam, makamu mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Ally Mohammed, amesema kuwa
lengo lao kubwa ni kutaka kupewa mikataba na posho, hivyo wanataka
kuonana na waziri wa uchukuzi na kushinikiza wageni kutoka nje ya nchi
kupewa kipaumbele cha kupatiwa ajira kuliko wazawa.
Wakati huohuo, Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, amesema kuwa anazo
taarifa za uwepo wa mabaharia hao na tayari amekwishafanya vikao viwili
na viongozi wao, hivyo malalamiko yao ni ya msingi na serikali tayari
inayafanyia kazi
0 comments:
Post a Comment