Wakazi
wa jiji la Dar es Salaam wamefurika katika ufukwe wa koko na kumpongeza
rais Dkt John Magufuli kwa uamuzi wake wa kutaka ufukwe huo uendelee
kuwa wa wananchi wote hususani wenye uwezo wa hali ya chini ili waweze
kufurahi ndani ya nchi yao.
ITV imetembelea katika ufukwe huo wa koko na kukuta zaidi ya watu
elfu 10 wakiwa wamepumzika na wengine wakiogelea wakisherehekea
mapumziko ya siku ya mwaka mpya ambapo wakizungumza na ITV wamesema rais
Magufuli ameonekana kujali zaidi wanyonge wenye uwezo mdogo na
kusisitiza kwa upande wao hawana uwezo kulipa fedha ili waweze kustarehe
katika fukwe hizo.
Kwa upande wao baadhi ya wafanyabiashara ndogondogo wameitaka
serikali kutoruhusu sehemu hiyo kuweka mifumo itakayotaka wananchi
kulipa kiingili kwa kuwa kufanya hivyo kutapunguza idadi ya wananchi
wanaotembelea ufukwe huo hali inayoweza kukwamisha biashara zao.
0 comments:
Post a Comment