Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji ameitaka Mamlaka
ya Mapato (TRA) mkoa wa Mbeya kuhakikisha inaanda mpango maalumu kwa
ajili kudhibiti mapato yanayopotea kutokana na kushamiri kwa biashara
ya ubadilishaji wa fedha kiholela katika mpaka wa Tunduma na Zambia.
Dk. Kijaji ametoa kauli hiyo Mkoani Mbeya baada ya kutembelea TRA
mkoani humo na kusema serikali imekuwa ikipoteza mapato mengi hasa
kutokana na kuwepo kwa biashara hiyo kiholela.
Amesema serikali lazima ijiendeshe yenyewe kwa kuongeza ukusanyaji wa
mapato sanjari na kuzuia mianya yote ya ukwepaji wa kodi pamoja na watu
wote kuhakikisha wanalipa
kodi.
Katika hatua nyingine Naibu waziri huyo ameuagiza uongozi wa TRA
katika mpaka wa Tunduma na Zambia kuhakikisha kuwa mizigo yote
inayosafirishwa kupitia mpaka huo inafanyiwa tathimini na kulipiwa kwa
muda usiozidi siku moja .

0 comments:
Post a Comment