Mji mmoja kaskazini mwa Italia unasherehekea kuzaliwa kwa mtoto wa kwanza tangu mapema miaka ya 1980.
Meya
wa mji wa Ostana, ulioko eneo lenye vilima la Piedmont, anasema
kuzaliwa kwa mtoto huyo ni “kutimia kwa ndoto” ya jamii ndogo inayoishi
katika mji huo.
Idadi ya watu katika mji huo imeshuka sana katika
kipindi cha miaka 100 iliyopita, na walikuwa wamesalia watu 84 pekee na
ni nusu yao pekee huishi katika mji huo bila kuhamahama, Gazeti la La
Tampa linasema.
Mtoto Pablo, aliyezaliwa katika hospitali moja mjini Turin amefikisha idadi ya watu mjini humo hadi 85 sasa.
Meya
Giacomo Lombardo anasema mji wa Ostana ulikuwa na watu 1,000 mapema
miaka ya 1900 lakini wakaanza kupungua baada ya Vita Vikuu vya Pili vya
Dunia.
"Watu walipungua zaidi kuanzia 1975, ambapo ni watoto 17
pekee waliozaliwa kati ya 1976 na 1987, ambapo mtoto wa mwisho –
mvulana- alizaliwa,” anasema.
Tangu wakati huo, hakuna mtoto mwingine aliyezaliwa hadi sasa mji huo ulipompokea Pablo.
Mji huo unajaribu kukabiliana na hali ya kushuka kwa idadi ya watu kwa kuunda nafasi za kazi.
Wazazi
wa Pablo, Silvia na Jose, walikuwa wamepanga kuhamia ng’ambo miaka
mitano iliyopita lakini ripoti zinasema waliamua kukaa baada ya kupewa
kazi.
Sherehe kubwa imeandaliwa mjini Ostana, kusherehekea
kuzaliwa kwa Pablo, na kwa mujibu wa La Stampa, sanamu ya korongo
imewekwa kwenye lango la kuingia mji kwa heshima yake.

0 comments:
Post a Comment