Akizungumza
Muda mfupi baada ya kuapishwa mbele ya Rais John Magufuli kuwa Katibu
Mkuu Wizara Ya Mali Asili na Utalii,Meja Jenerali Milanzi alisema ni
aibu Tanzania kuendelea kupoteza wanyama pori bila hatua stahiki
kuchukuliwa.
"Siwezi
kuvumilia kuona serikali ikishindwa kusimamia rasilimali za nchi
ambazo ndizo zinaoongeza idadi ya watalii nchini na pato la
taifa.Majangili wanaongozwa na uchu na uchoyo kwa watanzania wengine.
"Maliasili
zilizopo ni kwa ajili ya kuwanufaisha watanzania wote na kuliletea
sifa taifa letu.Ni aibu kuonyesha dalili za kushindwa katika mapambano
dhidi ya ujangili.Maliasili na utalii ndio kitovu cha mapato ya taifa,
kwani wanyama hasa wale adimu ndio huvutia watalii.
"Nitatumia
mbinu na uwezo wangu wa kijeshi kukabiliana na hilo,kwa sasa ni mapema
kusema lolote.Kuna mambo mengi ninatakiwa nijifunze kwanza,lakini
tutaangazia matatizo yote yanayoikabili wizara hii nyeti.
"Kuna
masuala ya vitalu vya uwindaji,kuna tatizo la wananchi kuwepo ndani ya
hifadhi za taifa;yote tutayaangazia pamoja na kuangalia namna ya kutoa
elimu kwa wananchi juu ya uhifadhi na ujangili." Alisema Meja Jenerali Milanzi.
chanzo mpekuzi huru

0 comments:
Post a Comment