MCHEKESHAJI mkongwe nchini, Amri Athumani ‘King Majuto’, amefunguka
na kudai kwamba kuna baadhi ya wasanii wa filamu wanafanya kazi zao bila
ya kuwa na lengo la kuelimisha jamii zinazowazunguka.
Msanii huyo amedai kwamba, wasanii wengi wapo kwa ajili ya
kufurahisha watu lakini wanasahau kwamba wanatakiwa kuelimisha jamii kwa
kuwa wao ni kioo cha jamii.
“Ukiangalia filamu zangu nakuwa nachekesha lakini nafundisha, ila
kuna wasanii wengine kazi yao kubwa ni kuchekesha katika kila filamu
lakini hawatumii muda wao kwa ajili ya kuelimisha,” alisema Majuto.
Mkongwe huyo amekuwa na idadi kubwa ya mashabiki kutokana na uwezo wake wa uigizaji.

0 comments:
Post a Comment