Saturday, January 9, 2016





IKULU ya Kenya imemlipua mwanasiasa maarufu wa nchi hiyo Raila Odinga kuwa amekuwa akiongoza kwa vitendo vya hujuma. Mbali ya hiyo, Ikulu imesema Raila na washirika wake wakuu, Kalonzo Musyoka na Moses Wetangula wanaandamwa na rekodi yao mbaya ya zamani kuhusiana na vitendo vya rushwa na kuwa walikuwa wakitumia ofi si za serikali kwa manufaa binafsi.

Habari zilisema, Ikulu juzi ilitupa makombora kwa Raila na kumhusisha na vitendo vya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka ikiwa ni kipindi kifupi baada ya kiongozi huyo kusema Serikali ya Muungano wa Jubilee, imeshindwa.

Katika kutupiana makombora baina ya pande hizo, Ikulu inaonekana kutayarisha video zilizorekodiwa maalumu kwa ajili ya kiongozi huyo wa Mungano wa Cord ambaye alikuwa madarakani katika uongozi uliopita.

Uongozi wote wa Cord ulighubikwa na vitendo vya rushwa na wahusika walitumia ofi si za umma kwa ajili ya kujinufaisha binafsi,ilisema sehemu ya taarifa dhidi ya Raila. Iliongeza kuwa: ìTulichojifunza kutoka kwa wapinzani ni matarajio yao makubwa ya kutumia ofi si za umma kama sehemu ya kupora mali ya umma.

Majibu hayo ambayo yanatokana na mtazamo wa Raila kuhusiana na uongozi wa Jubilee, yalitolewa na Kitengo cha Rais cha Mawasiliano, ambacho ni kwa ajili ya masuala ya Rais Uhuru Kenyatta, inaonyesha kuwa sasa vita baina ya wanasiasa hao vinapiganwa katika kiwango cha juu kabisa.

Raila, ambaye alikuwa waziri mkuu katika utawala uliopita, alihusishwa na kashfa ya uuzwaji wa mahindi kutoka hifadhi ya taifa na kuwa alitoa vibali kwa familia na marafi ki zake wa karibu. Pia, na viongozi wenzake waandamizi wamehusishwa na jinsi walivyosimamia Programu ya Kazi kwa Vijana.

Wakati akitupiwa tuhuma hizo, Raila naye katika siku za hivi karibuni amekuwa akiitupia shutuma za kuhusika na vitendo vya rushwa kwa serikali iliyopo madarakani. 

Mbinu mojawapo inayotumiwa na Muungano wa Jubilee ni kama vile kujaribu kukata miguu ya kiongozi huyo kwa kuibua hoja ambazo zilikuwa na utata.

0 comments:

Post a Comment