Star
wa Bongo Flavor Madee jana aliahidi kuchoma moja ya gari lake endapo
timu ya Chelsea ingeifunga Arsenal kwenye mchezo wa Premier League jana
January 24 kwenye uwanja wa Emirates.Mchezo huo ulimalizika kwa Arsenal
kukubali kipigo cha goli 1-0 lilifungwa na Diego Costa dakika ya 23
kipindi cha kwanza na kudumu kwa dakika zote za mchezo huo.
Wadau
mbalimbali walikuwa na hamu ya kujua kama Madee alitimiza azma yake ya
kulitia kibiriti gari lake baada ya Chelsea kuituliza Arsenal kwenye
uwanja wake wa nyumbani na kuendeleza rekodi ya kutopoteza mechi nyingi
za ligi dhidi ya mahasimu wao wa jiji la London.
Leo
asubuhi Madee ame-post ujumbe kwenye account yake ya tweeter akijibu
maswali mengi kuhusu matokeo ya mechi ya Arsenal vs Chelsea na yeye
kuchoma gari lake.
Star
huyo ameandika ujumbe unaosomeka hivi: “Sina utajiri huo mpaka kufikia
hatua ya kuchoma gari. Hata kama ningekuwa tajiri vipi, nisingefanya
upumbavu huo”.
Jana
Madee hakupokea simu ambazo alikuwa akipigiwa na wadau mbalimbali
wakitaka kujua kama ametekeleza ahadi yake ya kuchoma gari aliyoitoa
kabla ya mchezo huo.
Jana
kupitia account yake ya instagram Madee alipost ujumbe kwamba, endapo
Chelsea ikiifunga Arsenal atachoma moto gari lake moja.
0 comments:
Post a Comment