Thursday, January 14, 2016



Kumbe picha za ‘harusi’ za Linex zimezua kizaazaa hadi nyumbani kwao Kigoma.  Picha za ‘harusi’ za Linex zilizosambaa mtandaoni zilizua kizaazaa ambapo wazazi na ndugu zake walimpigia simu na kumuuliza kwanini ameoa kimya kimya bila kuwashirikisha ndugu na wazazi wake.

 ‘’Unajua zile picha zilikuwa na ‘antetion’kubwa sana na kiukweli siku’plan’ kutengeneza ‘antetion’ ya wimbo mimi nilikuwa natengeneza kava ya wimbo wangu kwahiyo nilivyopost picha ya kwanza nimevaa pete na msichana nilishangaa jinsi watu walivyoipokea nilivyoweka ya pili ikawa balaa,’’Alisema Linex. 

‘’Nikashangaa ndugu zangu wakaanza kunipigia simu tena kiugomvi wakaniuliza kwanini nimefanya kitu kikubwa kama hicho bila kuwashirikisha,Kiukweli sijaoa ni picha za kava ya ngoma yangu mpya iitwayo ‘’Kwa hela,’’Alisema Linex.

0 comments:

Post a Comment