| Mbwana Samatta. |
Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya
Tanzania na klabu ya TP Mazembe ya Congo DR, Mbwana Samatta leo hii
anatarajiwa kuwasili nchini Nigeria kuhudhuria sherehe za utoaji wa tuzo
kwa wachezaji bora barani Afrika zitakazofanyika katika mji wa Abuja
Alhamisi tarehe 7 Januari...,
Samatta anawania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika pamoja na mlinda mlango wa TP Mazembe, Robert Kidiaba (Congo DR) na mshambuliaji wa Etoile du Sahel Baghdad Boundjah (Algeria).
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine ameandamana na Samatta kuhudhuria sherehe hizo.
0 comments:
Post a Comment