Friday, January 8, 2016

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa na Mbunge wa Bunge la Jamhuri wa Donge kutokea Zanzibar Mh. Sadifa
jana ghafla bin vuu ameishangaza Dunia kwa kufunga ndoa ya kushitukizia na Msanii Maarufu nchini na Mjane wa Msanii Sajuki yaani Wastara. Habari hii ilitojitokeza usiku wa jana kwenye mitandao ya kijamii bongo ilipokewa kwa mshituko mkubwa sana kuzingatia kwamba mpaka wiki iliyopita Wastara alikuwa bado ni mpenzi halali wa Boyfriend wake wa zamani na wa siku nyingi sana Mtangazaji maarufu wa TV kwa jina la Bond. Blogu ya Wananchi ilipompigia Bond kutaka kujua ya undani hakuwa na la kusema zaidi ya kuesma anamuombea furaha tu mpenzi wake wa siku nyingi Wastara ambaye sasa anakuwa mke wa Nne wa Mjumbe huyo mtata wa Kamati Kuu ya CCM Taifa. Ndoa yake ya 4 imekuja wakati Rais mpya Magufuli anajitahidi kuhimiza wananchi kupunguza matumizi, ndio maana imekuwa ni gumzo kubwa sana hapa mjini leo kwamba Mjumbe huyo wa Kamati Kuu CCM Taifa kweli ataweza kuwatunza wake 4 kwa wakati mmoja kwa mshahara wa Serikali?

0 comments:

Post a Comment