Tuesday, January 19, 2016

Mkuu Mpya wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh. Makalla leo amefanya ziara wilaya ya Hai kwa kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Barabara ya Rundugai na kuweka jiwe la msingi ujenzi wa madarasa 2 sekondari ya Kia
Aidha amefanya kikao cha pamoja na Kamati ya Ulinzi na usalama, madiwani, watendaji kata na Vijiji , waratibu Elimu kata na wakuu wa idara na ameelekeza yafuatayo
1.Mkuu wa wilaya ya Hai na watalaam wa Afya wakutane na viongozi wa wilaya ya simanjriro ili kuthibiti ugonjwa wa kipindupindu ambao wagonjwa wote wakioripotiwa wanatoka wilaya ya Simanjaro. Mkoa wa kilimanjaro umedhibiti ugonjwa wa kipindupindu hakuna mtu aliyefariki na wagonjwa wakioripotiwa wanatoka simanjriro na wote wametibiwa na wamebaki wagonjwa 2 tu
2. Ameagiza Uongozi wa wilaya na madiwani kukomesha ubadhirifu. Amehoji ni kwa vipi halmashauri hiyo inapata hati safi miaka 8 mfululizo lakini ndiyo inaongoza kwa ubadhirifu wa Fedha za umma ambapo watumishi zaidi ya nane wameshafukuzwa kazi na wengine wapo mahakamani.












0 comments:

Post a Comment