Posted by Williammalecela.com on Thursday, January 14, 2016
Mkuu
Mpya wa Mkoa wa Kilimanjaro afanya ziara manispaa ya Moshi kwa kukagua
ujenzi mradi wa Maji utakaohudumia watu 9000 wa kata ya Languo, Rau na
kuboroloni na kuagiza kasi ya ujenzi iongezwe . Mradi unagharimu Fedha
sh 675m Amezindua Maabara Shule ya sekondari ya Anna Mkapa na
kuutaka viongozi wa manispaa kupitia mapato ya ndani kukamilisha vifaa
vilivyobaki Aidha katika kikao cha majumuisho Kamati ya Ulinzi ya
wilaya, madiwani, waratibu wa Elimu Kata na watendaji wa kata ametoa
maelekezo yafuatayo 1. Mkoa wa kilimanjaro ktk Matokeo ya darasa la
saba umeshika nafasi ya 4 kitaifa. Ameagiza watoto wote waliofaulu
waende Shule na watoro wote wasakwe. Elimu ni bure na Fedha za kutoa
Elimu bure mkoa umepokea sh 998,935,000. Ameagiza wakuu wa Shule kutumia
Fedha hizo kwa uangalifu 2.Ameagiza kila halmashauri kupanda miti
milioni moja ili kurejesha mkoa kilimanjaro katika mazingira mazuri,
amepiga marufuku uchafuzi wa mazingira na kuharibifu wa vyanzo vya Maji
na wote waliojenga na kufanya shughuli za kijamii ktk vyanzo vya Maji
kwa mujibu wa sheria ya mazingira waondoke mara moja 3. Ameagiza
wote waliojitwalia maeneo ya wazi wararudishe mara moja amehaidi
kupambana na wote wenye tamaa ya kujitwalia maeneo ya wazi ikiwemo
viwanja vya Shule 4.Amepiga marufuku uchomaji wa matofali katikati ya jamii na kusababisha madhara
0 comments:
Post a Comment