Posted by Williammalecela.com on Friday, January 15, 2016
 |
Mkuu Mpya wa mkoa wa Kilimanjaro Mh. Amos Makalla leo amefanya ziara halmashauri ya Moshi kwa
kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Maabara Shule ya sekondari Dr chami,
.Amekagua mradi mkubwa wa Maji inajengwa kutoka chanzo cha mto Gona
utakaohudumia wananchi wa kata ya njiapanda wapatao 25,000. Mradi
unagharimu Fedha sh 800 milioni smbao unafadhiliwa na ujerumani kupitia
shirika la TPP trust na serikali ya Tanzania Aidha amefanya kikao na watendaji wa Vijiji, waratibu wa Elimu kata, madiwani, wakuu wa idara na Kamati ya Ulinzi na usalama . 1. Amewataka viongozi watendaji kuthibiti ulevi , uuuzaji wa pombe haramu na unywaji pombe wakati wa KAZI
2. Amekemea uharibifu wa mazingira katika vyanzo vya Maji na ukataji
miti na uharibifu wa msitu wa mlima Kilimanjaro kwa kulinda msitu huo
theluji ya mlima kilimanjaro imeanza kuongezeka |
0 comments:
Post a Comment