Monday, January 25, 2016

Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh. Amos Makalla wilayani Mwanga leo Ameweka jiwe la msingi ujenzi wa hostel ya wasichana sekondari ya Mandaka, uzinduzi studio baadaye itakuwa Redio na television itwayo KIMS tv and Redio station na ujenzi wa dampo
Katika kikao cha watendaji wa vijijini, kata , tarafa, madiwani na Kamati ya Ulinzi na usalama ameelekeza yafuatayo
1. Amekemea tabia ya kuuza ardhi kiholela vijijini bila kufuata utaratibu. Mahitaji ya ardhi yanaongezeka lakini ardhi haiongekezki hivyo tuwe makini
2. Ameiagiza Kamati za maafa wilaya zote kujipanga kufuatia taarifa toka Mamlaka ya hali ya hewa kuhusu mvua Nyingi zinazotarajiwa kunyesha hivyo wananchi wote wanapaswa wachukue tahadhari
3.Ameagiza halmashauri zote kuwa na dampo za kisasa kwani suala la usafi ni ajenda ya kudumu na takataka zisombwe kwa wakati na zitupwe kwenye dampo rasmi siyo porini au makorongoni








0 comments:

Post a Comment