NA MWANDISHI WETU, Uwazi
DAR ES SALAAM: Yule mgonjwa anayeaminika ndiye aliyetoa siri ya kuharibika kwa mashine za CT Scan na MRI Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa Rais Dk. John Magufuli na wiki iliyopita kudai amelazwa chini, Chacha Makenge, amesababisha mapya kuibuka.
Wakizungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita, maofisa
uhusiano wa Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (Moi), Frank Matua na
Patrick Mvungi kwa nyakati tofauti, walisema kuwa, mgonjwa huyo hakuwa
na tatizo lolote la kiafya na alisharuhusiwa kuondoka hospitalini hapo.
Akaongeza kuwa, baada ya kuonekana hana tatizo, aliruhusiwa kwenda
nyumbani lakini anakataa akidai hana pa kwenda. Ndipo alipowaeleza
maofisa hao kuwa ana familia ipo Mugumu, Serengeti mkoani Mara.
“Tulimtafutia tiketi ya basi na fedha za matumizi ili aende kwao
lakini siku ya safari alikataa kwenda akisema anakwenda msibani. Pia
akaelekeza kuwa fedha tulizomtengea kwa safari wapewe wagonjwa wengine
ziwasaidie.
“Baada ya siku kadhaa, akarudi hapa Moi. Tulipomkumbusha kuwa amesharuhusiwa, alikataa kuondoka, hatukumshusha kitandani.
Wagonjwa wanaokataa kwenda makwao baada ya kuruhusiwa hapa hospitali
wapo wengi na hatuwafukuzi, in humanitarian ground (kibinadamu),
tunawapa huduma zote za chakula na malazi kwa gharama za serikali hadi
utaratibu mwingine utakapofanyika,” alisema Matua.
Alifafanua kuwa, baada ya kuona Chacha anawasumbua kwa tabia zake
mbalimbali, walimchunguza, wakagundua alishawahi kuwa na jalada katika
wodi ya wagonjwa wenye matatizo ya akili Muhimbili, hivyo sasa wanafanya
utaratibu mwingine wa kumsaidia.
Wiki iliyopita, gazeti hili lilikwenda Muhimbili, Taasisi ya Mifupa
na Mishipa ya Fahamu (Moi) na kumkuta Chacha akiwa amelala chini na
akadai ameshushwa kitandani.
Kwa kuona kuwa uwepo wake pale unaweza kusababisha kumchafua Rais
Magufuli aliyesimamia zoezi la kupatikana kwa vitanda, gazeti hili
liliandika habari zake ili uongozi wa hospitali hiyo uchukue hatua bila
kujua kwamba huko nyuma mgonjwa huyo aliwahi kufunguliwa jalada kwenye
wodi ya wagonjwa wa akili.
Hata hivyo, maofisa uhusiano wa taasisi hiyo hawakupatikana wakati
huo kuzungumzia tukio hilo lililowaacha midomo wazi watu walioingia
wodini humo siku hiyo ya tukio.

Sasa kama wao madaktari wana uhakika kuwa huyo mgonjwa wa akili kwanini anachanganywa na wagonjwa wa kawaida au mpaka aje kuua mgonjwa mwenzake? Sasa huo si ndio uzembe wenyewe? Kama mueshimiwa raisi asingefanya ziara ya kushtukiza haya yote tungeyajua wapi?
ReplyDelete