Video Queen maarufu Bongo, Asha Salum ‘Kidoa’.
Video Queen maarufu Bongo, Asha Salum ‘Kidoa’ amemtangazia vita mpenzi
wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarinah Hassan ‘Zari’ akidai
atafanya kila njia amnase msanii huyo.
Rafiki wa karibu wa Kidoa aliyeomba jina lake lisiandikwe gazetini
alidai kuwa, Kidoa alikuwa akimpenda sana Diamond hata kabla ya kuwa na
Zari ndiyo maana ana ndoto za kuwa naye.
“Kidoa anamzimia sana Diamond, achilia mbali kumpenda kutokana na
kazi yake ya muziki lakini pia kimapenzi, maana kuna wakati anakosa raha
kabisa anapowaona Zari na Diamond wakiwa kimahaba,” anadai mtoa habari
huyo.
0 comments:
Post a Comment