Kundi la RA ambalo
ni la Kikristo nchini Ghana linatarajia kuzindua kmtandao wa
kijamii ambao unatajwa kuwa mtakatifu kinyume na uliozoeleka wa Facebook...
Kundi hilo la Ra, lenye jina, LoveRealm, limesema kwamba mitandao ya kijamii imejaa picha zenye maudhui ya utupu na ukatili.
Lakini kundi hilo limejinasibu kuwa mtandao wao ujao utawasaidia wale ambao walikuwa na mahangaiko ya kulinda imani zao dhidi ya mitandao isiyokuwa na maadili na mtandao huo utasaidia washirika wake kutubu dhambi miongoni mwao.
Kwa sasa mtandao huo mtakatifu umekwisha waalika maelfu ya wafuatiliaji Wakristo wafanye majaribio ya kushiriki katika tovuti hiyo katika kituo cha Pentekoste katika mji mkuu, Accra.
0 comments:
Post a Comment