Anayefuata kutumbuliwa this time ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Juma Assad. Nimesoma ripoti inayotuhumu ofisi yake, iliyoenda kwa JPM ina "ukakasi" mwingi;
Ripoti hiyo inasema tangu Assad ateuliwe kushika wadhifa huo Novemba 5, 2014 na kuapishwa Desemba 2 mwaka huo na Rais mstaafu Jakaya Kikwete, ofisi yake imebariki mambo kadhaa kinyume na maadili na majukumu yake.
1. Ukarabati wa nyumba ya Serikali Plot namba 973 iliyopo Mikocheni, Dar es Salaam inayotumiwa na CAG.
Kwa mujibu wa taratibu, nyumba zote za Serikali zipo chini ya Wakala wa Majengo ya Serikali (TBA) na ukarabati hufanywa na kusimamiwa na wakala huyo, lakini ya CAG aliamua kufanya ukarabati mwenyewe.
Alitafuta kampuni yake (M/SAfriq - Engineering and Construction Co. Ltd) na kuilipa jumla ya shilingi mil 281.8 kabla hata ya kuanza kazi. Kabla ya Profesa Assad kuingia katika nyumba hiyo, ilikuwa ikitumiwa na CAG aliyestaafu, Ludovick Utouh. Ikumbukwe nyumba hiyohiyo ilikarabatiwa kwa Shilingi Bil.1.2 miaka mitatu iliyopita.
2. Professa Assad kanunua "furniture" za ndani kwa Mil.18 kutoka UAE (Dubai), akazisafirisha kwa Mil.7 na kuzilipia kodi Mil.9. Jumla "Furniture" hizo zimegharimu Mil.34 hadi zinaingizwa nyumbani kwake tarehe 27 December mwaka 2014 siku ya Jumamosi (saa 5 asubuhi).
3. Profesa Assad amenunua Shangingi la kutembelea kwa ajili ya matumizi ya CAG (TOYOTA LAND CRUISER GX-V8 200 HIGH) kwa gharama ya US $ 84,480.05 (Sawa na Mil.170). Manunuzi hayo yalifanywa kinyume na utaratibu. Pesa za kununua gari hiyo zililipwa kupitia Account Na. 0250095100500 iliyopo benki ya CRDB Bank (Plc) Tawi la Vijana, Dar es Salaam.
4. CAG na watendaji wake 11 walijiandikia safari ya kikazi ya siku 10 kwenda Seychelles. Profesa Assad na wenzie walisafiri Septemba 11, mwaka 2015. Lakini walitumia siku moja tu kukaa Sychelles kwa ajili ya mkutano wa kikazi. Na siku zilizobaki walienda "kula bata" Dubai, na China hadi September Septemba 22, waliporejea Dar es Salaam.!
Source:- Facebook

0 comments:
Post a Comment