| Waziri wa Mambo ya nchi za nje wa Saud Arabia,Adel al Djubeir |
Viongozi wa Ryadh wametangaza kusitisha mawasiliano ya angani na uhusiano wa kibiashara pamoja na jamhuri ya kiislam ya Iran.
Akiombwa aelezee masharti gani yanahitajika ili kurejesha uhusiano kati ya nchi hizo mbili,balozi wa Saud Arabia katika Umoja wa Mataifa,Abdallah bin Yahya Al-Mouallimi amesema: "Sisi na Iran hatukuzaliwa tuwe maaduwi .Tabia ya serikali ya Iran ya kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyengine na hasa za kiarabu,ikiwa ni pamoja na nchi yetu ndio sababu ya kuchukua msimamo huu."
JUHUDI ZA UPATANISHI
| Maandamano mjini Teheran dhidi ya kunyongwa sheikh Nimr al Nimr nchini Saud Arabia |
Mzozo wa Saud Arabia na Iran unafufua uhasama wa jadi kati ya nchi hizo mbili katika wakati ambapo vita vinapamba moto nchini Iraq,Syria na Yemen uhasama unaosababishwa na kiu cha kuania masilahi kati ya washiya na wasunni.
Saud Arabia inakamata nafasi muhimu katika juhudi za kuwaleta pamoja wanamgambo wa upinzani wanaoweza kushiriki katika mazungumzo ya amani pamoja na serikali ya rais Bashar al Assad wa Syria.
Umoja wa Mataifa ungependelea mazungumzo hayo ya amani yaanze january 25 ijayo mjini Geneva..
Marekani imeanza kuwasiliana na viongozi wa Ryadh na Teheran ili kuwasihi wavute subira-amesema hayo msemaji wa ikulu ya Marekani.
DIE LINKE WANATAKA BIASHARA YA SILAHA ISITISHWE PAMOJA NA SAUDI ARABIA
| Kiongozi wa chama cha siasa kali za mrengo wa kushoto die Linke,Sahra Wagenknecht |
Serikali kuu ya Ujerumani imezitolea wito serikali za Saud Arabia na Iran ziketi na kujadiliana.Msemaji wa serikali Steffen Seibert ameutaja uhusiano wa nchi hizo mbili kuwa na umuhimu mkubwa katika kupatiwa ufumbuzi mizozo ya Syria na Yemen.
Upande wa upinzani unaitaka serikali kuu isitishe ushirikiano wa aina pekee pamoja na Saud Arabia ili kuweza kuwa mpatanishi kati ya Iran na Saud Arabia.Kundi la chama cha siasa kali za mrengo wa kushoto die Linke linakwenda umbali wa kutaka isitishwe biashara ya silaha kwa ncnhi hiyo ya kifalme.
0 comments:
Post a Comment