Peter Okoye wa P Square amefungua kampuni ya kusimamia wanamichezo na ameanza na wachezaji wa mpira wa miguu.
Kampuni hii imepewa jina P-Classic Football Management na imeshapata viongozi na watu wanaofanya kazi kuhakikisha inakuwa kampuni kubwa.
Peter amekuwa mfadhili mzuri wa timu ya mpira ya Omole FC kwa miaka mitano sasa na amesha wafadhili wachezaji wawili kwenda Europe kujifunza soka na wengine wamepangwa kwenda mwaka huu.
Peter Okoye ndio huyu mwenye kipindi cha tv cha “Dance Nigeria With Peter” kilichoanzishwa na kutazamwa zaidi mwaka 2015.Peter ana mke anaitwa Lola na watoto wawili Cameron na Aliona.
0 comments:
Post a Comment