Tuesday, January 19, 2016

drake-obama-kendrickdrake-obama-kendrick
Kutoka kushoto ni Drake, rais Barack Obama na Kendrick Lamar.
KWA mara nyingine tena rais wa Marekani, Barack Obama ameonesha kumkubali rapa wa Compton, Kendrick Lamar baada ya kufunguka kuwa rapa huyo anamfunika rapa mwenzake Drake kwenye kuchana (rap battle).

Obama amekaririwa akisema hayo kwenye intavyu maalum na mtandao maarufu duniani wa wa YouTube iliyofanyika Ijumaa (January 15). Intavyu iliyokuwa na hoja ya kujadili mambo kadha ya nchi hiyo na baadaye kuwajadili wakali wawili wa kuchana (Meek Mill na Drake).
Lakini mtangazaji aliyekluwa akiongoza intavyu hiyo aliuliza swali la kizushi kwa Obama huku akichombeza.
“Nani anaweza kushinda endapo Kendrick lamar na Drake wakipambanishwa kuchana?” Aliuliza mtangazaji huyo.
Obama buila kupepesa macho akafunguka palepale, “Kura yangu nitampa Kendrick.” Alijibu Obama kwa kumpendezeza Kendrick anayewania vipengele 11 kwenye tuzo za Grammy.
Akitaja sababu ya yeye kumkubali zaidi Kendrick kuliko Drake, rais Obama alisema, “Nadhani Drake ni mtumbuizaji (entertainer), lakini mashairi ya Kendrick ni…. Albamu yake ya mwisho  (To Pimp a Butterfly) ndiyo albamu bora, nadhani ni mwka jana.”.

0 comments:

Post a Comment