Rais mstaafu wa awamu ya nne Mhe Dkt Jakaya
Mrisho Kikwete ametunukiwa Shahada ya heshima ya udaktari wa falsafa wa
mahusiano ya kimataifa Leo Jijini Dar es Salaam katika mahafaliya 30 ya
Chuo Kikuu Huria Tanzania.
Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amesema
amefarijika sana kutunukiwa shahada hiyo ya heshima itolewayo na Chuo
kikuu Huria Tanzania kwa watu ambao wametoa mchango katika maendeleo
katika jamii kupitia nafasi zao kiutendaji.
“Naipokea heshima hii toka Chuo
Kikuu Huria Tanzania kwa moyo mmoja kwani wameona mchango ambao nimeutoa
nilipokuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Awamu ya Nne
hivyo basi nitaendeleza mahusiano na ushirikiano kimataifa”.Alisema Mhe.
Dkt Kikwete.
Mbali na Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kuna
baadhi ya maraisi na wakuu mbalimbali duniani waliwahi kupata Shahada za
heshima toka Chuo Kikuu Huria Tanzania ambao ni Rais wa Awamu ya kwanza
wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais wa Awamu ya pili
Alhaji Ali Hassan Mwinyi, Rais wa Awamu ya tatu Benjamin William Mkapa,
Rais wa zamani wa Afrika ya Kusini Hayati Nelson Mandela na Dkt
Koichiro Mastuura Mkurugenz iwa UNESCO.
Chuo kikuu Huria cha Tanzania kimetoa jumla
ya wahitimu 69 wawili Shahada maalum na 67 ni Shahada, Stahahada na
Astashahada, ambapo Shahada ya uzamivu ni wahitimu watatu, Shahada ya
uzamili ni wahitimu 20, Shahada wahitimu 22,Stashahada wahitimu 15 na
Astashahada wahitimu 6.

0 comments:
Post a Comment