RAIS John Magufuli amempongeza Rais mstaafu, Jakaya Kikwete kwa
kuteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon kuunda jopo la
watu mashuhuri.
Watu hao watamshauri Kimoon juu ya namna bora ya kuendeleza na
kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu, hususan katika afya ya uzazi
ya mama na mtoto.
Hayo yamo kwenye taarifa kwa vyombo vya habari, iliyotolewa na Kurugenzi wa Mawasiliano, Ikulu, jijini Dar es Salaam jana.
Ilisema jopo hilo la watu mashuhuri, linaongozwa na wenyeviti wenza,
Rais wa Chile, Michelle Bachelet na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam
Desalegn.
Rais mstaafu Kikwete na Rais mstaafu wa Finland, Tarja Halonen wameteuliwa kuwa wenyeviti mbadala.
“Kuteuliwa kwa Rais Kikwete kuwa miongoni mwa jopo la kumshauri
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kumeijengea heshima Tanzania na
kumechochea matumaini ya mafanikio ya kukabiliana na changamoto za afya
ya mama na mtoto, hususan kwa nchi zinazoendelea, ikiwemo Tanzania,”
ilisema taarifa hiyo ya Ikulu.

0 comments:
Post a Comment