Serikali
imeelezea azma yake ya kuurejesha muswada wa huduma za vyombo vya
habari Bungeni huku ikisisitiza Muswada huo utarejeshwa baada ya
majadiliano na maafikiano ya kina na wadau.
azma hiyo ya serikali imetolewa jijini Dar es Salaam na wazairi wa
habari, utamaduni, sanaa na michezo Mh.Napen Nauye ambapo amesema mpango
wa serikali ni kuhakikisha muswada huo unakuwa shirikishi ili kuijenga
tasnia ya habari nchini.
Katika mkutano huo uliowashirikisha wahariri kutoka vyombo
mbalimbali vya habari nchini, wahariri hao licha ya kupongeza azma hiyo
ya serikali wamesema ni vema serikali ihahakikisha majadiliano ya
upatikanaji sheria bora ya habari yanafanikiwa.
Mh.Nape amewahakikishia wadau wa tasnia ya habari kuwa serikali ya
awamu ya tano inania thabiti ya kuurejesha muswada wa huduma za vyombo
vya habari ulio na uwiano sawa kati ya seriklai na wadau hao ili
kuiimarisha tasinia hiyo muhimu ya habari hapa nchini.
Mapema june 2015 serikali iliridhia kuondolewa kwa muswada wa
sheria ya haki ya kupata habari ya ya mwaka 2015 baada ya wadau wa
habari kuugomea muswada huo kwakutokukidhi matwaka ya tasnia ya habari
hapa nchini.
0 comments:
Post a Comment