Posted by Williammalecela.com on Monday, January 11, 2016
Gazeti la Jambo leo na Raia Tanzania
yote kwa pamoja ambayo yanatoka kwa siku, yako mbioni kufungiwa na
Serikali ya Rais John magufuli.
Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya
Ofisi ya msajili wa Magazeti nchini,ambazo mtandao huu umezipata
zinasema kwa sasa ofisi hiyo ya msajili itafikia uamuzi baada
ya kubainika Magazeti hayo yamekiuka sheria ya magazeti ya mwaka 1976.
Makosa ambayo yanadaiwa kufanywa na
magazeti hayo ni ile ya wamiliki wa magazeti hayo kuyauza kinyemela bila
ya hata kuishirikisha ofisi ya msajili wa magazeti nchini kama sheria
ya magazeti inavyokata,pia kuchangia kuikosesha serikali mapato kutokana
na uuzwaji huo .
Taarifa za magazeti hayo kuuzwa
zilipotiwa wiki mbili zilizopita kuwa,Gazeti la Jambo leo ambalo mwanzo
lilimilikiwa na Kampuni ya Jambo Concepts Tanzania ambapo kwa sasa
inadaiwa kuwa kampuni hiyo imeliuza Gazeti hilo kwa Kampuni ya Quality
Media Group ambayo inamilikiwa na Mwenyekiti wa Klabu ya mpira ya
Yanga,Yusuf Manji.
Mbali na hilo,Gazeti la Raia Tanzania
pia nalo limeuzwa pia kutoka kwa Bodi ya wanahisa wa Gazeti la Raia
Mwema ambapo kwa sasa Bodi hiyo imeliuza Gazeti hilo kwa Kampuni ya TSN
Super Market, inadaiwa sababu ya Bodi ya wamiliki wa Raia Tanzania
kuliiuza gazeti hilo baada ya kuporomoka kimauzo.
“Ninachokwambia magazeti haya lazima
yafungiwe ndugu,maana yamekiuka sheria ya magazeti ambayo inawataka
walete taarifa ofisi ya msajili,lakini hawa hajafanya hivyo ,tena
wameikosesha mapato serikali maana wanauziana magazeti kinyemela huku
serikali haipati mapato,nakuhakikishia lazima yafungiwe tu.”kimesema
chanzo chetu kilichopo ndani ya ofisi ya msajili wa Magazeti.
0 comments:
Post a Comment