Wakaazi wa mji wa California walilazimika kutafuta njia mbadala baada ya sili mmoja kukwama barabarani mchana kutwa.
Wenyeji
wa jimbo hilo walipiga ripoti kwa maafisa wa kuelekeza magari
wakiripoti kuwepo kwa mnyama huyo kwenye barabara ya Highway 37 katika
jimbo la Sonoma .
Polisi na wanahabari walipigwa na butwaa walipofika katika eneo hilo na kumuona sili (elephant seal) amekwama barabrani.
Waliwaita
maafisa wa huduma ya wanyama pori ambao hawakuwa na maelezo ni vipi
mnyama huyo mwenye takriban kilo 500 alipatikana katikati ya barabara
kuu.
Licha ya kushtuliwa kupigiwa honi na hata kumwagiwa maji, sili huyo hakubanduka.
Mwishowe waliamua kumdunga sindano ya kumlewesha iliwanyanyue wamwondoe barabarani.
Maafisa wa Marine Mammal Center hatimaye walimbeba na kumfanyia vipimo vya siha yake na kugundua kuwa alikuwa ni mjamzito.
Alipelekwa
kwenye hifadhi ya wanyama yaP oint Reyes National Seashore ambapo
atahudumiwa hadi atakapojifungua kisha arejeshwe baharini.
0 comments:
Post a Comment