SPIKA wa Bunge la Uganda, Rebecca Kadaga (Mb), ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika
(CWP) Kimataifa ameziasa nchi wanachama wa Sekretarieti ya CWP kuendelea
kuwathamini wanawake kwa kuwapa vipaumbele vya ushiriki katika ngazi za
maamuzi pamoja na kuwaenzi wanawake waliotoa mchango wa maendeleo ya
nchi zao.
Spika Kadaga aliyasema hayo juzi Dar es Salaam wakati akifunga rasmi
warsha ya siku mbili iliyohusu kujadili ushiriki wa wanawake katika
ngazi za maamuzi ili kubuni mbinu na mikakati ya kuongeza idadi ya
wanawake katika ngazi za siasa na kijamii.
Kadaga alisema nchi wanachama hazina budi kuthamini mchango mkubwa wa
wanawake katika masuala ya kijamii pamoja na kisiasa, hivyo kuna haja
ya kuwaenzi kwa kutunza nyaraka zao muhimu ikiwemo kuwaendeleza wanawake
kielimu ili kuweza kuleta maendeleo katika nchi husika.

0 comments:
Post a Comment